Mshukiwa wa ugaidi taabani

Mshukiwa wa ugaidi taabani

Na RICHARD MUNGUTI

MSHUKIWA wa kundi la ugaidi Al Shabaab alipatikana na kesi ya kujibu na Mahakama ya Milimani Nairobi Jumatatu.

Hakimu mwandamizi Bernard Ochoi alimpata na kesi ya kujibu Job Kimathi Gitonga almaarufu Khaleed  almaarufu Kim katika mashtaka ya kupatikana na video za masomo ya itikadi kali.

Hata hivyo Bw Ochoi alitupilia mbali shtaka kwamba Gitonga alikuwa mwanachama wa kundila kigaidi la Al Shabaab.. Alitupilia mbali mashtaka mengine matatu.

Bw Ochoi aliamuru  Gitonga aliyekamatwa na kushtakiwa Mei 30, 2019 ajitetee katika mashtaka ya kupatikana na filamu za kushinikiza ugaidi.

Hakimu huyo alisema upande wa mashtaka ulioongozwa na  Bw James Gachoka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kuwezesha Gitonga kujitetea kwa kupatikana na video 14 katika jengo la Norwich Union jijini Nairobi za mafunzo za itikadi kali.

Mshtakiwa anayewakilishwa na Chacha Mwita alieleza  mahakama atawaita mashahidi watatu.

Atajitetea akiwa upande wa mashahidi ndipo aulizwe maswali na kiongozi wa mashtaka. Mshtakiwa ataaingia kizimbani Desemba 16, 2021.

You can share this post!

Tuambiwe ukweli, nani huchoma soko la Gikomba? Wakenya...

Westham tayari kung’ang’ania ligi kuu uingereza

T L