Habari

Mshukiwa wa uhalifu auawa Kayole

March 25th, 2020 1 min read

Na MWANDISHI WETU

WYCLIFF Vincent Oduor ‘Vinii’ anayedaiwa kuhusika katika wizi wa Sh72m kutoka kwa ATM Nairobi West mwaka 2019 ameuawa kwa risasi Kayole, imesema Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI).

Ufyatulianaji ulitokea baina ya maafisa wa polisi na genge la washukiwa watatu wa uhalifu watatu katika eneo la Kayole Junction, Nairobi usiku wa kuamkia leo Jumatatu, DCI imesema kupitia ukurasa wa akaunti yake ya Twitter.