Habari Mseto

Msichana akana kumuua mwanamume wa miaka 20

October 2nd, 2020 1 min read

Na ANGELINE OCHIENG 

Msichana wa miaka 17 alikana mashtaka ya kumuua mwanamume wa miaka 20 kwenye mahakama ya Kisumu kufuatia mzozo uliotokea katikati ya mwezi uliopita..

Msichana huyo na mwanamume huyo wanasemekana kuwa walikuwwa kwenye uhusiano uliokuwa na matatizo.

Mashataka yalisema kwwamba msichana huyo alimuua mwanamume huyo Septemba 7  kwenye soko la  Apoko Nyakach kaunti ya Kisumu.

Mshukiwa huyo anasemekana kumdunga mnwanamume huyo kutumia kisu cha jikoni kabla ya kutoroka kutoka eneo la tukio.

Alikamatwa bada ya babayake mshukiwwa kuripoti kisa hicho wa kituo cha polisi  cha Pap Onditi.

Mwanamume huyo alifariki alipokuwa akipokea matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya Kericho.

Mshichaananhuyo alifanyiwa unguzi wa kiakili kwenye hospitali ya Jaramoingi Oginga Odinga  na kupatikana kwamba kwamba laikuwa sawa kujibu mashataka.

Alifika mbele ya jaji Fred Ochieng na kukana mashtaka hayo. Msichana huyo aliiomba korti imwachilie kwa dhamana ya chini kwani alikuwa wa umri wa chini.

Korti ilimchangua mwanasheria Byrone Menzes kumwakilisha mshukiwa The court appointed lawyer Byrone Menzes to represent the suspect during trial.

Kesi hiyo itasikizwa tena Oktoba 29 .