Habari Mseto

Msiingize siasa kwa sukari ya sumu, wanasiasa waonywa

June 20th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Wanasiasa wameonywa dhidi ya kufanya suala la sukari ghushi na operesheni dhidi ya la kisiasa.

Msemaji wa serikali Eric Kiraithe Jumatatu aliwataka wanasiasa wanaojua wafanyibiashara walioko katika biashara ya bidhaa ghushi.

Alisema hiyo wakati wa mkutano na wanahabari Mombasa baada ya Kiongozi wa walio wengi Bunge Aden Duale kusema kwamba Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i na Waziri wa Fedha Henry Rotich wanafaa kuwajibika.

Msemaji huyo alisema, “Maoni yoyote ya kisiasa ni ya kugeuza mambo yalivyo na hayana haja na ni juhudi zilizokunywa maji.”

Duale alidai kuwa wafanyibiashara walaghai wa sukari wanalindwa na kwamba kampuni kadhaa zimepewa idhini ya kuagiza sukari nchini bila kutozwa ushuru.

Kulingana na Duale, Matiang’i analenga watu wasio katika vita dhidi ya sukari ghushi nchini.

Alidai kuwa alijua mtu anayehusika katika uagizaji huo, kwa kusema ndiye yule yule anayehusika katika ukataji haramu wa miti.