Michezo

Msimamo wa viwango vya soka kimataifa wakati wa corona

April 11th, 2020 1 min read

Na CHRIS ADUNGO

HUKU mashindano ya soka yakiwa yamesitishwa kwa muda duniani kote kutokana na virusi vya corona, hakuna mabadiliko makubwa kwenye msimamo mpya wa mataifa katika orodha ya viwango bora vya mwezi Machi iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Vipute vingi vya kimataifa, zikiwemo mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia na mapambano mengi ya haiba kubwa vimekuwa vikiahirishwa kwa muda usiojulikana tangu mwanzoni mwa Machi 2020.

Msimamo mpya uliotangazwa jana uliathiriwa na michuano minne pekee; yote ikiwa ya kirafiki. Mabadiliko makubwa zaidi yalishuhudiwa na Sudan Kusini waliopanda kwa nafasi tano zaidi na kuingia katika nafasi ya 168 sawa na Bermuda walioshuka kwa nafasi saba zaidi baada ya kupigwa 2-0 na Jamaica mnamo Machi 13, 2020.

Katika orodha ya mataifa 10-bora inayofungwa na Colombia, Ubelgiji ni ya kwanza ikifuatwa na Ufaransa, Brazil, Uingereza na Uruguay mtawalia. Croatia inashikilia nafasi ya sita ikifuatwa na Ureno, Uhispania na Argentina kwa usanjari huo.

Senegal ni taifa la kwanza barani Afrika likifuatwa na Tunisia, Nigeria, Algeria na Morocco mtawalia. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inafunga orodha ya 10-bora barani Afrika nyuma ya Mali, Cameroon, Misri na Ghana mtawalia.

Tunisia, Algeria, Morocco, Misri na Qatar ndivyo vikosi vitano-bora vya Uarabuni.

10-BORA DUNIANI:

· 1. Ubelgiji (1)

· 2. Ufaransa (2)

· 3. Brazil (3)

· 4. Uingereza (4)

· 5. Uruguay (5)

· 6. Croatia (6)

· 7. Ureno (7)

· 8. Uhispania (8)

· 9. Argentina (9)

· 10. Colombia (10)

10-BORA BARANI AFRIKA:

· 20. Senegal (20)

· 27. Tunisia (27)

· 31. Nigeria (31)

· 35. Algeria (35)

· 43. Morocco (43)

· 46. Ghana (47)

· 51. Misri (51)

· 53. Cameroon (53)

· 56. Mali (56)

· 56. DR Congo (56)

· 5-BORA UARABUNI:

· 27. Tunisia (27)

· 35. Algeria (35)

· 43. Morocco (43)

· 51. Misri (51)

· 55. Qatar (55)