Habari Mseto

Msiwakejeli waliopona corona – Serikali

June 9th, 2020 1 min read

NA BERNADINE MUTANU

Wizara ya Afya imeonya Wakenya dhidi ya kuwakejeli wagonjwa wa corona waliopona virusi hivyo, hali inayowaletea unyanyapaa.

Katika hotuba ya Jumanne Waziri Msaidizi wa Afya Rashid Aman alisema kwamba unyanyapaa unaweza kulemaza juhudi za matibabu na upimaji na kuweka kila mtu katika hatari ya kupata virusi hivyo.

Dkt Aman alisema kwamba kuna uwezekanao wa virusi hivyo kuongezeka siku za usoni huku miezi tatu ikikaribia kuisha kutoka kisa cha kwanza kuripotiwa humu nchini.

Virusi hivo vianendelea kusambaa kwa kasi humu nchini.