Habari MsetoSiasa

Msiwapake wakulima tope la vita vya Jubilee – Murkomen

May 28th, 2020 1 min read

NA IBRAHIM ORUKO

Maseneta wamekejeli hatua ya serikali ya kukoma kununua mazao ya wakulima wa humu nchini, wakisema hatua hiyo ni kuwaaadhibu wakulima na kuwa imechochewa na siasa.

Wizara ya Kilimo ilitangaza sera mpya, ikidai sera hizo zitajenga mazingira bora ya kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara kufanya maamuzi ya kilimobiashara.

Waziri wa Kilimo Peter Munya alisema kwamba uamuzi huo ni sehemu ya mabadiliko na mikakati ya ukuaji wa sekta ya kilimo ya 2019-2029 inayolenga kuhakikisha taifa limepata utoshelevu wa chakula.

“Hizi ni siasa. Waziri anafaa kutoa taarifa kueleza kilichoplekea kuundwa kwa sera hizo. Wakulima wa Bonde la Ufa wanaumia kutokana na miegemeo ya kisiasa. Nataka kumweleza Bw Munya kuwa wakulima hawafai kuhusishwa na vita nadi ya chama cha Jubilee,” akaema seneta wa Elgeyo-Marakwet Kipchumba Murkomen.

Chini ya sera hiyo mpya, wizara hiyo pia haitapendekeza bei inayofaa ya mbolea, mbegu na bidhaa zingine za shambani.

Serekali imekuwa ikinunua mbegu na nafaka kutoka kwa wakulima awali, lakini shughuli nzima imekuwa ikilemazwa na ufisadi.