Kimataifa

Mswizi aambukizwa Ebola Burundi

January 7th, 2019 1 min read

MASHIRIKA na CHARLES WASONGA

MWANAMUME mmoja anatibiwa kando na wagonjwa wengine katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Uppsala nchini Uswizi kwa kushukiwa kuambukiza ugonjwa hatari wa Ebola baada ya kutembelea Burundi, maafisa wa serikali wamesema.

Afisa Mkuu wa Matibabu katika hospitali hiyo alisema mwanamume huyo, wa umri wa makamo, ambaye amekuwa nchini Burundi kwa kipindi cha majuma matatu alionyesha dalili za kufuja damu, homa na kutapika damu.

Matokeo ya uchunguzi wake yalitarajia kutolewa baadaye siku ya Ijumaa..

Dalili za ugonjwa huo hatari na una virusi vinavyousababisha husambaa kwa kasi, huanza kuonekana baada ya wiki tatu.

Visa vya maradhi hayo havijaripotiwa nchini Burundi, lakini taifa hilo linapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambalo limekuwa likipambana na mkurupuko wake kwa zaidi ya miezi sita.

Ugonjwa huo imewaua watu 356 miongoni mwa 585 ambao wamethibitishwa kuambukizwa na virusi vyake.