MTG United yaiadhibu Limuru Starlets 4-0

MTG United yaiadhibu Limuru Starlets 4-0

Na Maureen Ongala

mongala@ke.nationmedia.com

VIPUSA wa timu ya kandanda ya MTG United jana waliwazaba wageni Limuru Starlets magoli 4-0 kwenye mechi ya ufunguzi wa msimu 2021/2022 wa ligi ya daraja la kwanza.

Mechi hiyo ilifanyika katika uwanja wa MTG, Kilifi. Mabao matatu yalifungwa na mshambuliaji Bi Nelly Jonathan mwenye umri wa miaka ishirini na moja katika dakika ya 53 na 63.

Mchezaji Rachael Sidi alifunga bao moja dakika ya 61.

Akizungumza na Taifa Leo Kocha wa MTG Bi Fathime Tibu alieleza furaha yake kwa timu yake kuzoa alama 3 katika mechi hiyo ya ufunguzi huku akisisitiza kuwa wana jukumu la kuhakikisha kuwa wanaingia katika ligi ya Premier msimu huu baada ya kupoteza na kushikilia nafasi ya pili kwa misimu miwili mtawalia.

“Wachezaje wajekaza vilivyo lakini pia nimegundua kuna upungu ambao ninastahili kuimasrisha kama kocha hasa upnade wa kumalizia kwa sababu tumepoteza nafasi mingi za kufunga mabao na pia wanahitaji kuwa na nguvu zaidi msimu huu,”akasema.

Bi Tibu alieleza ukosefu wa viungo vyake vya kutegemewa wakati wa ligi hizo kama chanzo kubwa cha matokeo mbaya ya timu yake ambao wengi wao huwa ni wanafunzi wa shule ya upili.

Hata hiyo alisema kuwa msimu huu amefanya mashaurino na shule husika ili kuhakikisha kuwa wanawapa wanafunzi hao nafasi ya kuhusika katika michwani msimu huu.

Wachezaji nane waliocheza katika mechi hiyo ya MTG na Limuru Sharlets ni wanafunzi.

“Tumekuwa tukikosa alama mbili ama moja katika misimu iliyopita licha ya timu yangu kuwa nzuri kwa sababu ilikuwa vigumu kukatiza masomo ya wanafunzi kwa sababu ya michezo hasa tunaposafiri kama Nairobi na nimekuwa nikikosa wachezaji wa ziada,”akasema

Hata hivyo mshambuliaji huyo matata mwenye umri wa miaka 21 ameweka wazi azma yake msimu huu baada ya kufunga ‘hatrick’ na kuipa timu yake ushindi.

“Naskia raha sana vile nimefunga ‘hatrick’ na nimejipanga kufunga zaidi ya yele nimefunga leo,”akasema Bi Jonathan.

Kulingana na Bw Jeremiah Sagom mkufunzi wa Limuru Starlets timu yake imepokezwa kichapo kufuatia kukumbwa na changamoto za usafiri pamoja na hali ya hewa kuwatatiza kwenye mchwano huo uliyopigwa saa nane mchana.

“Tumekubali kushindwa lakini wasichana wangu wanejitahidi licha ya uchovu wa safari ambapo wamekutana na wenyeji waliokuwa wamejiandaa vilivyo,”akasema.

Alitoa wito kwa wahisani kusaidia timu zinazokumbwa na changamoto ya fedha.

Licha ya changamoto hizo Sagom aliahidi kulipiza kisasi wakati timu yake itakapo pambana na Mombasa Olympic mjini Mombasa.

Timu ya MTG United watakutana na Mukuru Talents Academy leo saa nane mchana katika uwanja wa MTG mjini Kilifi.

Mwisho

You can share this post!

Mwanaume akata mkewe miguu kwa kumtoroka

Pigo kuu kwa Raila Uhuru akishindwa kudhibiti Mlima Kenya