Mtiririko wa vitushi na wahusika katika sura 10 – Chozi la Heri

Mtiririko wa vitushi na wahusika katika sura 10 – Chozi la Heri

MANDHARI ni usiku, njiani anakopita Shamsi akielekea kwake katika mtaa wa Kazikeni wanakoishi maskini, mtaa wa Afueni, Ridhaa wanakoishi matajiri (utabaka), Hospitali ya Mwanzo mpya (matumaini).

Wahusika – Shamsi, Ridhaa, Selume, Mwangeka, Meko, Apondi, Kipanga, Tuama, Tamira, Pete, Fungo, Nyangumi na walevi.

MTIRIRIKO WA VITUSHI

Shamsi alipita njiani huku akiimba katika kiza kikuu cha usiku. Wimbo huu unaangazia masuala mbalimbali yanayokumba jamii mathalan unywaji wa pombe haramu, matatizo ya umiliki wa ardhi, ukosefu wa ajira, mishahara duni, kuachishwa kazi kwa kutetea haki zao, ukosefu wa dawa na matibabu bora katika hospitali za kawaida.

Ridhaa aliyezoea kumsikia Shamshi akipita usiku huku akiimba anashangazwa na jinsi alivyohuzunika usiku huo. Ridhaa alikuwa amehamia mtaa wa Afueni (mtaa wa matajiri) baada ya Mwangeka kuoa. Shamshi naye aliishi katika mtaa wa mabanda wa Kazikeni uliokuwa karibu na Mtaa wa Afueni.

Selume ni muuguzi aliyekamilisha zamu yake ya kuwahudumia wagonjwa hospitalini Mwanzo Mpya.Alihudumu katika hospitali za umma awali alikokerwa na kuchushwa kushuhudia wagonjwa wakifa kwa ukosefu wa dawa zinazoishia katika hospitali za kibinafsi za wasimamizi wa hospitali.

Selume anamuonyesha muuguzi mwenzake,Meko mgonjwa mmoja wa kiume aliyeletwa hospitalilini na Wasamaria wema baada ya kupigwa kutokana na mzozo wa kupigania ardhi katika eneo la Tamuchungu.Kuna pia mgonjwa aliyekata roho kutokana na unywaji wa pombe haramu.Alikuwa mwanafunzi aliyesomea shahada ya uzamili.

Wanafunzi hawa hukata tamaa kutokana na hali duni ya maisha ya chuoni, gharama ya juu ya masomo na kukosekana kwa msaada kutoka kwa serikali; msaada wa elimu uliopo unatolewa kwa mapendeleo.Baadhi yao wanatumiwa na matajiri kulangua dawa za kulevya.

Tuama anazungumza na Meko na Selume jinsi alivyotoroka kwao ili aende kukeketwa kwa sababu ya shinikizo la rika. Wenzake waliaga dunia kwa kuvuja damu nyingi.Ilibidi Tuama akimbizwe hospitalini.Babake ni mwanaharakati dhidi ya ukeketaji wa wasichana lakini Tuama alienda kinyume naye.

Dadake Tuama aliyepitia kadhia hii,aliendelea na masomo hadi akahitimu kwa shahada. Tuama alidai kuwa hata yeye angeendelea na masomo ila anaogopa hatima yake kwa babake.

Selume anadai kuwa baada ya wasichana kukeketwa, wao huhiari kuolewa au kuozwa kwa lazima. Pia wao hukumbwa na hatari ya kuambukizwa magonjwa au kuvuja damu kupita kiasi. Wanamfikia Pete aliyelazwa. Pete ni mwana wa nne katika familia yenye watoto sita. Hajawahi kulelewa na wazazi wake. Pete alizaliwa nje ya ndoa,mamake alimpeleka alelewe na nyanyake.Alipofika darasa la saba, alipashwa tohara na kuozwa kuwa mke wa nne.

Pete alipitia masaibu mengi kutokana na unene wa mumewe, wivu wa wake wenza, kuchekwa na wanawawake hadi akaamua kutoroka mumewe Fungo miezi sita baada ya kupata mwana wa kwanza.

Tutaangazia hatima ya Pete na maudhui juma lijalo.

Joyce Nekesa

Kabsabet Boys High School

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Damaris Ketrai

TAMTHILIA: Maendelezo ya Onyesho la Tatu, Tendo la Kwanza...

T L