Habari Mseto

Mtoto, 12, afa maji kwa kutumbukia ndani ya josho la mifugo

May 6th, 2024 1 min read

NA GEORGE MUNENE

MWANAFUNZI wa umri wa miaka 12 alikufa alipoanguka kwenye josho la ng’ombe lililofurika maji kijijini Kiandegwa, Kaunti ya Kirinyaga.

Kwenye mkasa huo wa Jumapili, mvulana huyo, Dennis Murimi, alitoroka kutoka kanisa la Kenya Revival Church ambako wazazi wake walikuwa wakishiriki ibada, akajiunga na watoto wengine waliokuwa wakicheza karibu na josho hilo.

Aliteleza na kutumbukia ndani ya josho hilo lililokuwa limejaa.