Habari Mseto

Mtoto wa miaka 9 afariki baada ya jengo kuporomoka

June 10th, 2020 1 min read

NA VITALIS KIMUTAI

Mtoto wa miaka tisa alifariki baada ya nyumba ya ghorofa tatu kuanguka Jumanne jioni katika mji wa Kericho.

Majeruhi wengine wanne wamelazwa kwenye hospitali ya Kericho wakiwa na marejaha madogo.

Mwili huo ulipatikana saa tano baadaye wakati wa shughuli ya uokoaji iliyoendelezwa na polisi, maafisa wa kaunti ya Kericho wa kukabiliana na majanga na usaindizi wa umma.

“Mwathiriwa alipatikana ndani ya nyumba iliyobomoka na kutangazwa kuwa alikuwa amefariki baada ya kufika hospitalini Kericho,” alisema kamanda wa polisi Silas Gichunge .

Serikali ilitumia askari wa KDF kusaidia katika shughuli ya uokoaji na kutafuta watu ambao walikuwa wamebomokewa na nyumba..

Maafisa hao walifika hapo majioni na wakaendeleza shughuli ya uokoaji huku viogozi wa eneo hilo wakiwaamrisha wakazi kuhama kutoka kwa nyumba zilizo karibu na jumba hilo liliobomoka kabla ya Jumatano usiku.