Mudavadi, Weta wajianika kwa kususia hafla ya Raila

Mudavadi, Weta wajianika kwa kususia hafla ya Raila

Na BENSON MATHEKA

HATUA ya kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetangula ya kukataa mwaliko wa kiongozi wa ODM Raila Odinga kuhudhuria kongamano la Azimio la Umoja alilotangaza rasmi azma yake ya urais inaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa Muungano wa One Kenya Alliance (OKA).

Wadadisi wanasema kwamba kuhudhuria kwa mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi na kuashiria kumuidhinisha Bw Odinga kunathibitisha mpasuko na kushukiana katika OKA.

Japo kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka hakuhudhuria kongamano la Bw Odinga, wadadisi wanasema kuwa yeye na Bw Moi wako na ukuruba wa karibu na Bw Odinga tofauti na Bw Mudavadi na Bw Wetangula.

MIPANGO TOFAUTI

“Kilichojitokeza Ijumaa ni mpasuko wa wazi katika OKA. Ni thibitisho kwamba vinara wa Muungano huo hawana nia moia japo wamekuwa wakisisitiza kuwa wameungana. Ni thibitisho kuwa Mudavadi ana mipango yake tofauti na ya Bw Moi na Bw Musyoka ambaye alikuwa nje ya nchi Ijumaa,” asema mdadisi wa siasa Peter Kinama.

Bw Mudavadi alisema kwamba alialikwa kama kiongozi wa ANC na sio kinara wa OKA, na sawa na Bw Wetangula akasema hangehudhuria kwa kuwa alikuwa amepanga shughuli za kibinafsi.

Bw Kinama anasema japo uamuzi wa Bw Mudavadi na Wetangula unafaa kuheshimiwa, kauli za awali za wandani wake zinamsawiri kama hasimu mkubwa wa Bw Odinga.” Kumbuka wandani wake wamekuwa wakimkosoa Bw Musyoka na Bw Moi kwa kuhusiana na Bw Odinga.

Hivyo basi, kukataa kuhudhuria kikao cha Bw Odinga ni thibitisho kwamba hawafurahishwi na ushirikiano wa vinara wenzao katika OKA na Bw Odinga,” asema Bw Kinama. Akihutubu katika uwanja wa miichezo wa Kasarani Ijumaa kwenye kongamano ambalo Mudavadi na Wetangula walisusia, Bw Moi alidokeza kuwa OKA na Bw Odinga ni jeshi moja.

“Majeshi yetu ni moja. Raila anapopata nguvu sisi tunapata nguvu, tunapopata nguvu, Raila anapata nguvu pia,” alisema. Kulingana na mchanganuzi wa siasa Geff Kamwanah, kauli ya Bw Moi na ya Bw Mudavadi na washirika wake zinatofautiana.

“Ni wazi sasa katika OKA kuna kuchezeana shere. Kwamba Mudavadi na Wetangula wako kundi lao na Moi na Musyoka wako kundi lao sio siri,” asema Bw Kamwanah.

KUUNGANA NA RUTO

Mchanganuzi huyu anasema kuwa kuna uwezekano wa Bw Mudavadi na Wetangula kujiunga na Naibu Rais William Ruto huku Bw Musyoka na Moi wakiungana na Bw Odinga. “ Hisia zangu ni kwamba hawakutaka kuhudhuria kongamano la kumwidhinisha mpinzani wao kuwa chaguo la mrithi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, sidhani uamuzi wao ulikuwa wa busara ikizingatiwa kuwa ni msimu wa miungano ya kisiasa itakayoamua serikali itakayokuwa mamlakani baada ya uchaguzi mkuu ujao,” asema Bw Kamwanah. Bw Kinama anaongeza kuwa hatua ya Bw Mudavadi na Wetangula inaweza kuwaacha kwenye baridi ya kisiasa baada ya 2022 iwapo Bw Odinga atashinda urais na kuunda serikali.

“ Ni wakati wa wanasiasa hasa vigogo wa vyama vikubwa vya kisiasa kupima maamuzi yao vyema iwapo wanataka kuwa kwenye serikali ijayo. Ukichwa ngumu kwa yeyote asiye na idadi kubwa ya wafuasi unaweza kuwa hasara kwake, “ asema

You can share this post!

JAMVI: Uhatari wa ‘suti’ kwa Ruto, Raila

ODM kumenyana na UDA Bondeni

T L