Habari Mseto

Mulamwah adai atafichua sura ya mwanawe iwapo ‘atalipwa Sh100m’

March 2nd, 2024 1 min read

NA FRIDAH OKACHI

MCHEKESHAJI David Oyando, almaarufu Mulamwah amefichua kuwa atatoza Sh 100 milioni ili kufichua sura ya mwanawe.

Kwenye mahojiano ya hivi punde katika mtandao wa TikTok, baba huyo wa watoto wawili alisema atafanya mambo tofauti na watu mashuhuri kwa kufichua sura ya mwanawe.

Katika mahojiano ya hivi punde, mcheshi huyo alitaja kuwa anatamani kufanya mambo tofauti lakini yote yakienda sawa atatoza shilingi milioni 100 kwa ajili ya kufichua sura yake.

“Onyesho la uso litakuja kwa wakati ufaao…labda tutatoza milioni 100 kwa kuwa tutafanya mambo tofauti. Hakuna mpango wa kuashiria kuwa mtu mashuhuri, fanya tu kile unachoamini ni sawa na ufurahie na mashabiki hao watafurahia au watafurahia nawe,” alisema Mulamwah.

Februari 10, 2024 msanii huyo ambaye pia ni muuguzi kwa pamoja na mpenzi wake Ruth K walifanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Mulamwah na Ruth K walitangaza kuwasili kwa mtoto huyo huku wakisambaza video na picha za mtoto mchanga bila uso wake kuonekana.

“Mungu ni mkuu, hatimaye kijana wetu yuko hapa, mrithi yuko hapa, MFALME yuko – @oyando_jnr aka Kalamwah. Karibu duniani mwanangu, ni hisia nzuri zaidi duniani hatimaye kukuona na kukushika.

Wanandoa hao pia waliweza kumfungulia kurasa za kijamii, wakimtambulisha kwenye ulimwengu wa umaarufu kuwa Oyando_JNR ambaye ana mashabiki elfu kumi na saba.

Mwaka jana, mcheshi Eric Omondi alisema atafichua sura ya mwanawe pindi tu atakapopokezwa Sh50 milioni.

Baadaye alifichua sura ya mwanawe wakati alipomtambulisha kama Balozi wa Baby Shop Kenya (duka la nguo) mjini Nairobi ambalo linauza nguo za watoto.