Mulembe imani tele Mudavadi atawakwamua

Mulembe imani tele Mudavadi atawakwamua

NA DERICK LUVEGA

KINARA wa ANC Musalia Mudavadi anasubiriwa na kazi chungunzima katika eneo la nyumbani kwake magharibi mwa Kenya kufuatia uteuzi wake kama Waziri Mkuu.

Wakazi wa Magharibi wameanza kuandaa orodha ya miradi ambayo wangetaka aipatie kipaumbele mara tu atakapochukua usukani.

Ajenda za kwanza kabisa ni kuwekwa lami kwa barabara kuu, ufufuzi wa viwanda vilivyosambaratika na kuanzisha vipya pamoja na kuwapa ajira wakazi wa eneo hilo.

Orodha ya maendeleo vilevile inajumuisha utekelezaji wa mpango wa kujenga kiwanda cha granite katika Kaunti ya Vihiga pamoja na kiwanda cha kusafisha dhahabu katika Kaunti ya Kakamega.

Viongozi wa mashinani, hasa madiwani kutoka ngome yake ya Vihiga na chama cha ANC, walisema waziri mkuu mteule anapaswa kuitisha kikao cha washikadau pindi atakapochukua wajibu wake mpya.

Huku akimpongeza Rais William Ruto kwa kumteua Bw Mudavadi katika wajibu huo, Naibu Spika wa serikali ya Kaunti ya Vihiga, Eric Odei, Kiongozi wa Wachache Vincent Atsiaya, Diwano wa Busali Florence Kegode na Diwani Mteule Rita Atieno walisema Bw Mudavadi ameongoza eneo hilo kuingia serikalini baada ya miaka kumi ya kukaa nje.

  • Tags

You can share this post!

Ruto, Raila kumenyania kiongozi wa wengi bungeni

Kaunti kutoa ardhi zaidi kwa ajili ya upanzi wa kahawa

T L