‘Mulmulwas’ atangaza vita vya kumpokonya Poghisio useneta

‘Mulmulwas’ atangaza vita vya kumpokonya Poghisio useneta

Na OSCAR KAKAI

BW Dennis Ruto Kapchok aliyepata umaarufu mitandaoni baada ya Gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo kuibua kejeli kuhusu umbile lake, sasa anataka kuwania kiti cha useneta kinachoshikiliwa na Samuel Poghisio.

Akimtaja kama “Mulmulwas” , Prof Lonyangapuo alisema Bw Kapchok ni “Kijana mfupi round”, huwezi kujua tumbo ni wapi na mgongo ni wapi.

Katika video hiyo ya 2019, Profesa Lonyangapuo alikasirika kwamba Bw Kapchok alikuwa akikosoa serikali yake kwa kile alichotaja kama madai yasiyo na msingi.

Bw Kapchok, ambaye sasa ameungana na chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachohusishwa na Naibu Rais William Ruto, ameelezea matumaini ya kutwaa kiti cha useneta wa Pokot Magharibi.

Mwanasiasa huyo anasema lengo lake ni kuendeleza ajenda ya vijana. Bw Kapchok amemlaumu Seneta Poghisio kwa kufeli kuhakikisha kuwa kaunti ya Pokot Magharibi inatengewa fedha zaidi za maendeleo.

Bw Kapchok, ambaye tayari anadai kuwa kaimu seneta, alidai kuwa Bw Poghisio ametelekeza majukumu yake ya kufuatilia utendakazi wa Serikali ya Kaunti.

“Huwa hatumwoni. Ndio maana mimi ndiye kaimu seneta hapa,” akaeleza.

 

You can share this post!

Jambojet yatangaza mipango ya kuanzisha safari Goma na Lamu

ODM yaponda ‘usuhuba’ wa Ruto, Museveni