Mung’aro aahidi kuing’arisha Kilifi kimaendeleo

Mung’aro aahidi kuing’arisha Kilifi kimaendeleo

NA ALEX KALAMA

MSHINDI wa kinyang’anyiro cha ugavana katika Kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro ameahidi kuboresha kaunti hiyo na kuleta maendeleo kwa wakazi.

Akizungumza baada ya kupokea cheti chake cha ushindi kutoka kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Pwani mjini Kilifi, Mung’aro ameahidi kukabiliana na swala la ufisadi na uhaba wa dawa katika hospitali za kaunti ya Kilifi.

“Ushindi huu si ushindi wa Gideon Mung’aro bali ushindi huu ni ushindi wa watu wa Kilifi kwa sababu tutaboresha Kilifi. Nawaahidi ya kwamba Kilifi kuanzia leo haitakuwa kama ile Kilifi ya zamani. Itakuwa Kilifi ambayo ina maendeleo, itakuwa Kilifi ambayo haitakuwa na ufisadi, itakuwa Kilifi itakayopatia mkazi wa Kilifi dawa hospitalini, itakuwa Kilifi itakayopatia mkazi wa Kilifi maji safi, itakuwa Kilifi ambayo itakuza kilimo kwa watu wa Kilifi. Kwa hivyo, mimi ninakushukuruni na nikwaambieni kwamba sasa niko tayari kufanya kazi kwa roho yangu yote na nguvu zangu zote ili Kilifi hii isonge mbele,” akasema Bw Mung’aro.

Mung’aro alishinda wapinzani wake Aisha Jumwa na wakili George Kithi baada ya kupata kura 143,773.

MGOMBEA MWEGEMEO WA KISIASA KURA
1 Gideon Mung’aro

 

ODM 143,773
2 Aisha Jumwa UDA 65,893
3 George Kithi

 

PAA 64,326
4 Micheal Tinga Ford-Kenya 2,864
5 Esposito Kasoso Baya Mgombea wa Kujitegemea 2,709
6 Noti Kombe

 

USPK 2,574
7 Alphonce Dzombo Mbaru Safina 1,497

Vile vile seneta Stewart Madzayo pia ameweza kukihifadhi kiti chake baada ya kupata kura 144,740 na alizungumza baada ya kupewa cheti chake.

“Kwanza nataka kumshukuru Mwenyezi Mungu sana kwa kuweza kutuweka hai kwa kuweza kutuwezesha kufanya kampeni zetu kwa amani mpaka hivi sasa tumeweza kuibuka washindi. Ni kiwa hapa nataka kuwashukuru sana familia yangu nataka kuwashukuru sana zaidi sana watu wa Kilifi kwa imani waliyonayo juu yangu kwa kunirejesha tena kwa mara ya tatu. Nataka kuwaambia watu wa Kilifi nitatumia uwezo wangu akili yangu maarifa niliyonayo kuona ya kwamba ile kazi muliyonipa kuona ya kwamba watu wa Kilifi wamepata haki yao,na pesa zao zimekuja nyumbani kisawasawa nitafanya hivyo na bidii hiyo na nitatekeleza kwa mjibu wa vile ambavyo nyinyi mlivyonikabidhi mamlaka haya ya kuwa kiongozi wenu,” akasema Bw Madzayo.

Aidha Mwakilishi wa Kike Getrude Mbeyu pia alikinyakua tena kiti cha uwakilishi wa kike Kilifi kwa kuwashinda wapinzani wake Christine Zawadi na Juliet Riziki kwa kupata kura 111,039.

MGOMBEA CHAMA KURA
1 Getrude Mbeyu

 

ODM 111,039
2 Christine Zawadi

 

PAA 89,413
3 Juliet Riziki

 

UDA 49,111
4 Mary Luvuno

 

Mgombea wa Kujitegemea 21,769
5 Ephie Chari Wesa

 

Kadu-Asili 8,672
6 Moreen Atieno Mgombea wa Kujitegemea 2,339
  • Tags

You can share this post!

Utaratibu wa kukagua kura wachukua muda

Tufani ya UDA yamsomba mkuu wa kampeni za Raila

T L