Mung’aro afika kortini kujitetea asipoteze kiti

Mung’aro afika kortini kujitetea asipoteze kiti

NA ALEX KALAMA

GAVANA wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro jana Ijumaa alitoa ushahidi katika Mahakama Kuu ya Malindi ambako kesi iliwasilishwa ya kupinga ushindi wake na walalamishi wa chama cha PAA walioibuka nambari tatu kwenye kinyang’anyiro hicho katika uchaguzi mkuu uliopita.

Upande wa walalamishi ulikuwa ukiwakilishwa na wakili Edga Busiyega na wakili George Kithi ambaye pia alikuwa mgombea wa kiti hicho cha ugavana kwa tiketi ya chama cha PAA.

Mnamo Alhamisi, ilikuwa zamu ya afisa msimamizi wa uchaguzi kaunti ya Kilifi Hussein Gurre kutoa ushahidi wake kuhusiana na kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani na wapiga kura watatu wakipinga ushindi wa Mung’aro.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili Jaji Anne Adwera Onginjo ameeleza kuwa mahakama itaandaa kikao Februari 25, 2023 ili kutoa uamuzi wake iwapo masanduku ya kura yatafunguliwa na kuchunguza zaidi kura zilizopigwa katika uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

  • Tags

You can share this post!

Atletico wamsajili Memphis Depay kutoka Barcelona ili...

Macho kwa Ruth Chepng’etich watimkaji 400 wakishiriki...

T L