Habari za Kitaifa

Mung’aro aomboleza mwanajeshi Mpwani ambaye alifariki katika ajali

April 19th, 2024 1 min read

Na WACHIRA MWANGI

GAVANA wa Kilifi Gideon Mung’aro amemwomboleza Brigedia Jenerali Said Nzaro Swaleh ambaye aliaga dunia katika ajali ya ndege ya wanajeshi, iliyotokea katika eneo la Cheptulel, Pokot Magharibi na kuwaua watu tisa zaidi akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Francis Ogolla.

Katika mtandao wake wa kijamii Bw Mungaro alimwomboleza shujaa huyo Mpwani kutoka eneo la Kikambala, akituma rambirambi zake kwa familia, marafikina kikosi kizima cha majeshi wa ulinzi.

“Leo tunampumzisha Brigedia Swaleh anbaye ameacha ukumbusho wa huduma na kujitolea utakaokumbukwa na kuenziwa na wengi. Kumbukumbu zake ziendelee kututia moyo,” akasema Bw Mung’aro.