Musalia, Wetang’ula wamtetea Didmus

Musalia, Wetang’ula wamtetea Didmus

NA BRIAN OJAMAA

KIONGOZI wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetangula, wamemtetea Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa kuhusu sakata ya kuchapisha nembo za chama cha UDA kwenye gari la Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF).

Viongozi hao wawili wa mrengo wa Kenya Kwanza (KK) wameelezea kuwa anapigwa vita kisiasa.

Bw Barasa alijipata taabani, baada ya kuchapisha picha yake na ya Naibu wa Rais William Ruto, katika gari la NG-CDF, na hata kubadilisha nambari ya usajili wa gari hilo.

Wakizungumza katika eneo la Soysambu, Bungoma Kaskazini hapo jana, wawili hao walidai kuwa hata mgombea urais wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga, alikuwa akitumia magari ya serikali katika kampeni zake.

Walitaka polisi kumchunguza pia Bw Odinga kabla ya kumshukia Bw Barasa.

“Serikali itueleze ni kwa nini Bw Raila Odinga anatumia magari yenye nambari za usajili za KCY,” alisema Bw Wetang’ula.

Bw Wetangula alidai kuwa tangu kupatana kwa Bw Odinga na rais Uhuru, kinara huyo wa chama cha ODM amekuwa akitumia ndege na magari ya serikali.

“Viongozi waliopo katika Azimio hawajaulizwa kuhusu magari ya serikali. Kabla ya Barasa, serikali irudishe magari yote ya serikali ambazo tunaziona kwenye kampeni,” alisema Bw Mudavadi.

Bw Barasa alieleza kuwa hatatishwa na serikali kwani ipo katika siku zake za mwisho.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Viongozi waache kuingiza siasa katika mambo...

Tedros kuongoza WHO kwa miaka mingine mitano

T L