Museveni akemea mapinduzi Burkina Faso

Museveni akemea mapinduzi Burkina Faso

Na MASHIRIKA

KAMPALA, Uganda

RAIS Yoweri Museveni ameshutumu vikali mapinduzi yaliyotekelezwa nchini Burkina Faso dhidi ya serikali ya Rais Roch Marc Christian Kabore.

Rais Museveni aliyekuwa akizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 36 tangu atwae hatamu za uongozi wa Uganda, alisema nchi za Afrika ya Magharibi zinafaa kujifunza kutoka kwake kuhusu namna ya kuzima wanaopanga mapinduzi.

“Wengi wa viongozi wa kiraia wanashindwa kuunda jeshi thabiti hivyo wanakuwa katika hatari ya kupinduliwa,” akasema Rais Museveni.

“Ndani ya miaka 10 iliyopita, takribani nchi 10 zimepinduliwa katika eneo la Afrika ya Magharibi. Hatufai kuruhusu hili kufanyika. Hao wanajeshi wanapofanya mapinduzi hawaulizwi chochote na raia kwa sababu hawakuchaguliwa,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Vijana waapa kuunga Raila

Kimbunga Ana chaua 50 nchi jirani na Bahari Hindi

T L