Habari Mseto

Museveni atangaza siku ya kuombea corona

August 27th, 2020 1 min read

NA Jonathan Kamoga

Rais wa Uganda Bw Yoweri Museveni ametangaza Jumamosi kuwa siku ya maombi nchini humo kufuatia kuongezeka kwa virusi vya corona siku za hivi karibuni.

Nchi hiyo ilirekodi idadi ya visa vya corona vya juu zaidi Jumamosi.

Alhamisi  Wizara ya Afya ilitangaza visa 155 vya corona dakika chache baada ya Rais Museveni kutangaza Jmuamosi kuwa  siku ya maombi huku akiwaomba Waganda waiombee Uganda Mungu aiondolee janga hilo.

Kwenye mtandao wa Twitter Bw Museveni alisema kwamba alifikia hatua hiyo baada ya mwananchi mmoja kumuomba aweke siku ya mombi huku akidai kwamba alionyeshwa maoni na Mungu akimwambia waweke siku ya maombi nchini.

“Mwananchi mmoja alikuja kwangu na kuniambia kwamba  aliambiwa na mungu tuweke siku ya maombi nchini,ili mungu atuondolee janga hili la corona,” alisema Bw Museveni.

Uganda kwa sasa imerekodi visa 2,679 kufikia Alhamisi na vifo 28. Waliopona virusi vya  corona  ni watu 1,268.

TAFSIRI: FAUSTINE NGILA