Musyoka akoleza urafiki wa kisiasa na Lenku

Musyoka akoleza urafiki wa kisiasa na Lenku

Na STANLEY NGOTHO

KIONGOZI wa Wiper Kalonzo Musyoka wikendi alikita kambi katika Kaunti ya Kajiado kusaka uungwaji kuhusu ndoto yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Bw Musyoka pia aliwasihi wakazi wa kaunti hiyo yenye makabila mengi kumpigia kura gavana Joseph Ole Lenku katika uchaguzi huo wa 2022 akisema amefaulu kuunganisha jamii hizo.

Wakati huu Mbw Musyoka na Lenku ni marafiki wa kisiasa, hali ambayo imechangia jumbe kadhaa za watu kutoka jamii ya Wakamba kumtembelea Gavana Lenku katika muda wa mwaka mmoja uliopita.

Katika uchaguzi mkuu wa 2017, Bw Musyoka na wenzake wa vyama tanzu vya muungano wa Nasa walimuunga mkono Dkt David Nkedienye wa ODM aliyetetea kiti hicho baada ya kuhudumu kuanzia 2013.

Lakini Bw Ole Lenku aliyewania kwa chama tawala cha Jubilee ndiye aliyeibuka mshindi.

Hatua ya Bw Musyoka kumuunga Bw Ole Lenku sasa inatarajiwa kugeuzwa siasa katika kaunti hiyo yenye wapigakura 70,000 kutoka jamii ya Wakamba.

You can share this post!

Wabunge wa maeneo kame wataka NG-CDF zaidi

Raila amsuta Ruto kulialia ndani ya serikali