Muuzaji bidhaa za hospitali apewa muda kulipa deni la Sh883,000

Muuzaji bidhaa za hospitali apewa muda kulipa deni la Sh883,000

Na RICHARD MUNGUTI

MUUZAJI bidhaa za hospitali alipewa hadi Novemba 2021 kulipa kampuni inayomdai Sh883,000.

Bw Godfrey Otieno Ouma aliomba hakimu mwandamizi Bernard Ochoi muda alipe kampuni ya Zydui Limited iliyomshtaki kupokea bidhaa kwa njia ya undanganyifu.Kupitia kwa wakili Nick Omari mshtakiwa aliomba apewe muda asuluhishe suala hilo na walalamishi.

“Mshtakiwa anaomba mahakama impe muda alipe pesa anazodaiwa.Tayari ameweka mikakati ya kuzilipa,” alisema Bw Omari.Wakili huyo aliwasilisha kortini hundi tatu alizokuwa ameandikia walalamishi akieleza muda atakaochukua kulipa pesa hizo.

Mahakama ilimruhusu hadi Novemba 2021 awe amelipia pesa hizo.Shtaka dhidi ya mshtakiwa ni kuwa kati ya  Septemba 2019 na Novemba 2019 katika  Zydus Limited katika jengo Caribean iliyoko jijini Nairobi akiwa na nia ya kulaghai alipokea bidhaa za matibabu zilizo na thamani ya Sh 883,320 akidai alikuwa na uwezo wa kuzilipia.

Mshtakiwa alikanusha shtaka hilo na kuomba mahakama impe muda wa kulipa deni hilo.“Nimeombwa na walalamishi mshtakiwa apewe muda wa kulipa deni hilo,” Bw Ochoi alielezwa na  kiongozi wa mashtaka.

wakili Nick Omari anayemwakilisha Ouma…Picha/RICHARD MUNGUTI

Wakurugenzi wa kampuni hiyo ya Zydus Limited walikuwa kortini na kueleza mahakama hawataki kuendelea na kesi mradi mshtakiwa awalipe.Kesi hiyo itatajwa baada ya wiki mbili mshtakiwa akabidhiwe nakala za mashahidi.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 pesa tasilimu.Na wakati huo huo Bw Ochoi alifutilia mbali kibali cha kumtia nguvuni mshtakiwa kilichokuwa kimetolewa.Bw Omari alieleza mahakama Bw Ouma alikuwa nyumbani Siaya na hakupata nafasi ya kufika kortini kujibu shtaka wiki mbili zilizopita.

 

  • Tags

You can share this post!

NCIC yaonya wanasiasa wasiotaka kuona washindani ngomeni

SHINA LA UHAI: Kukabili athari za tabianchi: Denmark mfano...