Muuzaji nyama atozwa faini ya Sh1,000 au jela siku 14 kwa kuiba mnofu

Muuzaji nyama atozwa faini ya Sh1,000 au jela siku 14 kwa kuiba mnofu

Na RICHARD MUNGUTI

MFANYAKAZI katika duka la kuuza nyama aliyeiba kipande cha nyama ya kuku cha thamani ya Sh300 ametozwa faini ya Sh1,000 ama atumikie kifungo cha siku 14 gerezani.

Martin Mwai mwenye umri wa miaka 21 aliadhibiwa baada ya kukiri aliiba nyama hiyo kwa vile alikuwa na njaa ya kupindukia.

“Mheshimiwa ni ukweli niliiba nyama hii kwa vile nilikuwa na njaa,” Mwai alimweleza hakimu mkazi Mercy Thibaru.

Mwai alishtakiwa kuiba nyama hiyo kutoka kwa Quality Meat Packers mnamo Novemba 16, 2022.

Mmiliki wa duka hilo Bw Solomon Munyaka aliwajulisha habari za Mwai aliyeonekana kwa kamera akificha nyama hiyo kwa sweta yake.

Mshtakiwa alipelekwa kituo cha Mawe Mbili ambapo nyama hiyo ilitwaliwa na kurudishiwa mwenyewe baada ya kupigwa picha iliyotolewa kortini kama ushahidi.

Mshtakiwa aliyekuwa ameachiliwa kwa dhamana ya polisi ya Sh5,000 aliomba msamaha na kuomba korti imwachilie kwa dhamana.

Akipitisha hukumu hakimu alimuonya mshtakiwa dhidi ya kujiingiza kwa wizi kama huo.

“Hebu fikiria ukifungwa jela kwa sababu ya nyama ya Sh300? Usirudie kosa hili tena,” Thibaru alimuonya mshtakiwa kisha akamwamuru alipe faini ya Sh1,000 ama atumikie kifungo cha siku 14.

  • Tags

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Nyota Breel Embolo aongoza Uswisi...

Kenya yahimizwa kuchukua bima dhidi ya majanga

T L