Muyoti aanza kupanga City Stars upya

Muyoti aanza kupanga City Stars upya

NA RUTH AREGE

KOCHA wa klabu ya Nairobi City Stars ya Ligi Kuu ya Wanaume nchini (FKF-PL) Nicholas Muyoti amesema kuwa mashindano kama Elite Pre-Season Cup ya kujiandaa kwa msimu mpya yanahitajika kufanywa mara kwa mara.

Mashindano hayo yalifanyika kwa wiki mbili zilizopita ikiwa ni kufanya maandalizi ya msimu mpya.

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Nick Mwendwa wiki iliyopita alisema kuwa atapeana utaratibu wiki hii kuhusiana na msimu mpya.

Klabu ya Police FC ilitwaa kombe hilo na kupokea kikombe cha kibinafsi na Sh1 milioni.

“Nilifurahishwa na uzoefu ambao wachezaji wangu walikuwa nao wikendi iliyopita. Tunahitaji mashindano kama haya kupimana nguvu na pia kuwapa wachezaji nafasi ya kujitangaza kisoka,” aliongeza Muyoti.

Aliwapoongeza wachezaji wake kwa kuonyesha mchezo mzuri wakati wa mashindano hayo. Mabao ya David Simiyu na Marvin Nabwire yalikabidhi timu ya Police kombe siku ya Jumamosi katika mechi ya fainali iliyopigwa uwanjani Nyayo mjini Nairobi.

Muyoti ambaye ana idadi kubwa ya wachezaji chipukizi katika kikosi chake msimu huu, alibainisha kuwa michuano hiyo inawapa makinda uzoefu unaohitajika kucheza dhidi ya timu pinzani.

“Ilikuwa muhimu sana kwa wachezaji wangu kupata nafasi katika michuano hiyo. Nilitaka kuona ikiwa wanaweza kuendana na timu za ligi na sasa najua la kufanya kabla ya msimu kuanza,” aliongeza Muyoti.

  • Tags

You can share this post!

NDIVYO SIVYO: Matumizi yaliyozoeleka ya kauli ‘kwa...

VYAMA: Chama cha Uanahabari katika shule ya upili ya...

T L