Habari za Kitaifa

Mvua bado ipo!

May 22nd, 2024 1 min read

NA MWANDISHI WETU

KENYA na mataifa mengine sita ya Upembe wa Afrika yatashuhudia mvua kubwa kuliko kiwango cha kawaida kuanzia Juni hadi Septemba, ripoti ya utabiri wa hali ya hewa imesema.

Ripoti hiyo ni ya shirika la wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki (Igad).

Tayari Kenya imeshuhudia mafuriko kutokana na mvua kubwa maafa mengi yakiripotiwa Mai Mahiu katika Kaunti ya Nakuru.

Hii inamaanisha Wakenya wakae macho ili waepuke maafa yanayoweza kutokea.