Habari Mseto

Mwaka Mpya 2024 ulivyokaribishwa

January 1st, 2024 1 min read

NA SAMMY WAWERU

WAUMINI wa madhehebu mbalimbali nchini Jumapili, Desemba 31, 2023 walikongamana kwenye maeneo ya kuabudu kuukaribisha Mwaka Mpya 2023.

Wapo waliofuatilia kwenye vyombo vya habari hususan runinga zilizopeperusha moja kwa moja ibada kanisani na kwenye mitandao ya kijamii kama vile; Facebook Live na You – Tube.

Washirika wa Kanisa la Victor’s Assembly Nairobi wakikaribisha mwaka 2024. PICHA | BONFACE BOGITA

Mshale wa saa ulipogonga saa sita kamili, shangwe, vifijo na nderemo zilitanda angani.

Mbali na maeneo ya kuabudu, Wakenya wengine walifurika kwenye vituo vya burudani, vilabu na baa.

Miji, hasa Jiji la Nairobi fataki zilihinikiza hewani zikifuatwa na nderemo za furaha kuuona mwaka mpya 2024.

Maafisa wa polisi mitaa mbalimbali Nairobi walishika doria, kuhakikisha kuwa usalama umeimarishwa.

Maafisa wa polisi wakishika doria usiku wa kuamkia Januari 1, 2024. PICHA | BONFACE BOGITA