Kimataifa

Mwalimu afurushwa kwa kujichua mbele ya wanafunzi

January 10th, 2019 1 min read

MASHIRIKA na PETER MBURU

MWALIMU mmoja kutoka jimbo la Ohio nchini Marekani amekamatwa baada ya kupatikana akijipiga punyeto (hali ya kujisisimua sehemu nyeti ukiwa na uchu wa ngono) mbele ya wanafunzi alipokuwa darasani.

Bw Tracey Abraham, 41 alikuwa akifunza katika shule ya Creekside Middle, wakati wanafunzi walibaini “hulka isiyo ya kawaida lililokuwa likiendelea chini ya dawati la mwalimu huyo.”

Wanafunzi hao waliripoti kwa usimamizi wa shule na mara moja Abraham alitolewa kutoka darasa na jingo hilo.

Baadaye polisi walimshtaki kwa kufanya tabia zisizofaa katika eneo la umma. Aidha, alipigwa kalamu kutokana na hali hiyo ya kujichua mbele ya wanafunzi.

Kisa hicho kitaripotiwa katika idara ya elimu, japo jamaa mwenyewe aliachiliwa kutoka jela kulingana na rekodi za korti.

Lakini wasimamizi wa shule walisema kuwa mwalimu huyo hajaripotiwa kuwa na tabia yoyote ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi, ama kuwaonyesha uchi.

“Hatuna habari zozote za mwanafunzi kuonyeshwa uchi,” ujumbe wao ukasema.

Alipigwa marufuku kurejea katika wilaya hiyo kama mwalimu, baada ya kisa hicho kupangiwa kuripotiwa kwa idara ya elimu.