Habari Mseto

Mwalimu akana kumuua mumewe

October 20th, 2020 1 min read

NA SIMON CIURI

Aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya Icaciri alifika mbele ya mahakama ya Kiambu Jumatatu kujibu mashtaka ya kuhusika kwenye mauaji ya kumuua mumewe 2016.

Bi Jane Muthoni anashukiwa kupanga mauaji ya Bw Solomon Mwangi ambaye wakati wa kifo chake alikuwa mwalimu mkuu wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Kiru, Kaunti ya Murang’a.

Jumatatu Bi Muthoni alifika mbele ya mahakama Jumatatu akiwa na mshukiwa mwenzake Bw  Issac  Ng’ang’a. Wawili hao walionekana wakiwa wametulia .

Bi Muthhoni alisema kwamba bwanayake alitekwa nyara na wauaji ambao walikuwa wanadai Ramson.Alidai kwamba Novemba 6 alipokea simu kutoa wateka nyara hao na baadaye wakazima simu walipongudua kwamba walikuwa wanatafutwa na polisi kwani alikuwa ameripoti kisa hicho kwa polisi.

Lakini alishindwa kueleza kiasi cha pesa wateka nyara hao walichokuwa wakitaka.

Bi Muthoni aliiambia korti kwamba mumewe hakuuawa kati ya Novemba 6, 2016 na  Novemba 9, 2016 kama inavyodaiwa na korti kwani walizungumza naye wakati huo. Alikana kwamba alihusika kwenye kifo hicho.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA