Habari Mseto

Mwalimu mkuu Tononoka aangamia kwa corona

October 31st, 2020 1 min read

NA MOHAMED AHMED NA FAUSTINE NGILA

Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Tononoka amefariki kutokana na virusi vya corona kwenye hospitali ya Coast General Kaunti ya Mombasa.

Bw Mohammed Khamis aliafriki hospitalini humo alipokuwa akilazwa kwa wiki mbili baada ya kupatikana na virusi  vya corona.

Naibu wa mwalimu mkuu Benjamin Nzaro alithibitisha kifo cha Bw Khamis  Jumatatu asubuhi.

Bw  Khamis aliambukizwa virusi vya corona wiki ya kwanza ya shule kufunguliwa.

Shule hiyo ya Tononoka ilifunngwwa baada ya walimu wengine kupatikana na virusi vya corona.

Walimu na wanafunzi pia waliripotiwa kupata virusi vya corona huku wakilazimika kufunga shule.

Shule ya upili ya Star of the Sea pia ilifungwa baaada ya visa vya corona kuripotiwaa humo shuleni.

Duru za kuaminika zilisema kwamba watu wa nane kutoka shule ya upili ya Tononokaa waliripotiwa kuwa na virusi vya corona huku visa nne zikiripotisa shule ya upili ya Star of the Sea.

Kwenye barua iliyotolewa na shule ya Star ilisema kwamba shule hiyo ilifungwa kwa muda ili kuruhusu  shule hizo kunyunyuziwa dawa.

Bw Khamis amabye alikuwa amehamishwa kutoka shule ya upili ya  Lamu atazikwa kwa makaburi ya Kikowani.