Kimataifa

Mwalimu wa kike akiri kumlazimishia mtoto ngono

July 15th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWALIMU wa kike alifungwa miaka 20 gerezani, baada ya kukiri kuwa alifanya ngono na mvulana wa miaka 13 mara kadhaa.

Brittany Zamora, 28 alikiri mashtaka 10 ya kushiriki ngono na mtoto, mengine ya kumtesa mtoto, mawili ya kumpa mtoto vitu vya kingono na tabia za mahaba mbele ya umma.

Polisi waliambia korti kuwa Zamora alifanya ngono na mtoto huyo mara kadhaa katika gari lake na darasani, ikiwemo mara moja ambapo mtoto mwingine wa miaka 11 alikuwapo.

Hata hivyo, mwalimu huyo alijitetea mbele ya korti kuwa yeye ni mtu wa tabia nzuri na si hatari katika jamii.

Hata hivyo, mahakama haikuwa na huruma naye, ikimfunga miaka 20 ambapo haezikuachiliwa kabla ya kifungo hicho kukamilika, hata akionyesha tabia nzuri.

Zamora alikamatwa baada ya wazazi wa mtoto huyo kugundua kuwa hakuwa sawa kama kawaida yake, ndipo wakaamua kuweka kitu cha kumchunguza katika simu yake.

“Mbeleni alikuwa mtoto mzuri lakini mwalimu huyo aliutoa uzuri huo. Namchukia kwa kile alifanyia mtoto na familia yangu,” mamake mtoto huyo akaeleza korti.