Mwamerika Fred Kerley afuta muda bora wa mita 100 alioweka Omanyala

Mwamerika Fred Kerley afuta muda bora wa mita 100 alioweka Omanyala

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Afrika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala sasa si mtimkaji aliye na muda bora mwaka 2022 katika umbali huo.

Hiyo ni baada ya Mwamerika Fred Kerley kutimka mbio hizo za mita 100 kwa sekunde 9.83 kwenye mashindano yanayoendelea ya Amerika kuchagua kikosi cha Riadha za Dunia zitakazofanyika Julai 15-24 mjini Eugene jimboni Oregon.

Omanyala alishikilia muda bora mwaka huu baada ya kushinda duru ya Continental Tour ya Kip Keino Classic kwa sekunde 9.85 uwanjani Kasarani jijini Nairobi mnamo Mei 7.

Itakumbukwa kuwa Omanyala alinyakua taji hilo akiwamlemea wapinzani wake wa karibu Kerley na Isiah Young kutoka Amerika waliokamilisha kwa 9.92 na 10.13 mtawalia.

Omanyala anajivunia muda bora wa 9.77 aliopata akikamata nafasi ya pili nyuma ya Mwamerika Trayvon Bromell kwenye makala ya 2021 ya Kip Keino Classic uwanjani Kasarani.

Muda huo ni rekodi ya Afrika. Inspekta huyo wa polisi ameapa kuwapa mashabiki kitu cha kufurahia wakati Kenya itachagua timu yake ya kuelekea Oregon mnamo Juni 24-25 uwanjani Kasarani.

Anataka kutimka chini ya sekunde 10 hapo Jumamosi. Alinyakua taji la Afrika kwa sekunde 9.93 mnamo Juni 9 mjini Reduit, Mauritius.

  • Tags

You can share this post!

13 wauawa polisi wakipambana na wahalifu Mexico

Wakazi wa Kiambu wapatao 50,000 kupokea hatimiliki za ardhi

T L