Habari Mseto

Mwanabodaboda afariki pamoja na mteja wake ajalini

July 7th, 2020 1 min read

GEORGE ODIWUOR

Mwanabodaboda na abiria wake wamefariki baada ya ajali iliyotokea karibu na soko la Ringa Rachuonyo Mashariki kaunti ya Homabay baada ya kugongwa na lori lililokuwa limeendeshwa kwa kasi.

Abiria mwingine aliyekuwa kwenye bodaboda hiyo aliumia vibaya sana kwenye ajali hiyo iliyootokea kwenye barabara ya Katito-Oyugi Jumamosi jioni.

Mwendeshaji huyo wa bodaboda alitambulika kama Kevin Omondi mwenye miaka 20,huku abiria hao wakitambulika kama ,Sophine Anyago miaka 23.

Walioshuudia walisema kwamba Omondi alikuwa ameendesha bodaboda hio kutoka Mikayi kuelekea kwenye soko ya Ringa akiwa na abiria wawili.

Lori iliyowangoga ilikuwa ikielekea shemu moja na bodaboda hio.

Kamanda wa polisi wa Rachuonyo Mashariki alisema kwamba bodaboda hio iligogwa kutoka nyumba na lori hilo lilokuwa likifanya kazi kwenye mradi kwa kutengeneza barabara.

“Mwendeshaji huyo na abiria mmoja walikufa papohapo huku abiria mwingine akikibizwa hospitali akiwa na marejaha,”alisema.

Polisi aliwahimiza waendeshaji bodaboda kuwa makini wakitumia hio njia inayopita magari yanayotumika katika ujenzi wa barabara.

“Kuna mradi unaendelea wa ujenzi wa barabara na waendeshaji bodaboda wanapaswa kuwa makini kwasababu kuna machini zinaendeshwa na wafanyakazi wanaojenga barabara ,”alisema Bw Barasa..

Miili ya hao wawili ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya kaunti ndogo ya Rachuonyo Kusini.