Mwanabodaboda apigwa faini ya Sh11,000

Mwanabodaboda apigwa faini ya Sh11,000

Na RICHARD MUNGUTI

MWENDESHAJI piki piki alitozwa faini ya Sh11,000 kwa kuiendesha bila leseni. Samuel Wanyonyi alikiri mbele ya hakimu mwandamizi Bi Esther Boke mashtaka manne dhidi yake.

Wanyonyi alikiri aliendesha piki piki katika eneo la Kibera bila leseni.

Kiongozi wa mashtaka Allan Mogere alisema mshtakiwa alisimamishwa na polisi na alipoitishwa leseni ya kuendesha piki piki “hakuwa nayo.”

“Mbona uliendesha pikipiki bila leseni,” mshtakiwa aliulizwa na hakimu.

“Ni kweli niliendesha pikipiki bila leseni kwa vile niko na watoto wanne ninaowatunza. Wawili ni wangu na wawili ni wa ndugu yangu aliyefariki. Sasa wote wanahitaji chakula.Singeweza kusubiri watoto wafe njaa,” alisema Wanyonyi.

Kwa kila kosa kati ya hao manne mshtakiwa alitozwa faini ama atumikie kifungo cha miezi miwili.

  • Tags

You can share this post!

Mhubiri Nyeri achoma karatasi za kutangaza huduma za waganga

TANZIA: Mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza afariki