Habari Mseto

Mwanachuo akana madai ya unajisi

August 18th, 2020 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAFUNZI wa chuo kikuu cha Kenyatta University alishtakiwa kwa kumdhulumu kimapenzi msichana wa miaka 15 katika kaunti ndogo ya Kasarani Nairobi.

Bw Cyrus Thairu Maina, anayefanya somo la Hesabati na Sayansi katika chuo kikuu hicho cha Kenyatta alikabiliwa na mashtaka mawili.

Shtaka la kwanza lilisema Thairu alimtendea aibu msichana huyo mlalamishimwenye umri wa miaka 15 kwa kumtia kidole katika nyeti yake.

Shtaka la pili lilikuwa mnamo Agosti 15, 2020 alikabiliwa na shtaka kuwa alimtendea aibu mlalamishi kwa kuguza sehemu zake nyeti.

Mshtakiwa aliomba mshtakiwa aachiliwe kwa dhamana isiyo ya kiwango cha juu akidai “ni mwanafunzi na bila shaka atafika mahakamani wakati wa kusikizwa kwa kesi.”

Kiongozi wa mashtaka Bw George Obiri alisema hakuna stakabadhi zozote kuonyesha mshtakiwa ni mwanfunzi wa chuo kikuu.

“Mshtakiwa yuko tayari kuwasilisha stakabadhi kutyoka KU kuthibitisha ni mwanafunzi katika chuo hicho,” wakili anayemwakilisha Thairu alimweleza hakimu mwandamizi Bw Charles Mwaniki Kamau.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000.

Kesi itatajwa mnamo Agosti 31,2020.