Mwanachuo ashtakiwa kwa kutuma picha za ngono kwa mtoto wa kike

Mwanachuo ashtakiwa kwa kutuma picha za ngono kwa mtoto wa kike

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAFUNZI katika chuo cha Kabete Vetlab alishtakiwa Jumanne kwa kumtumia msichana wa miaka 14 picha za wanaume wakiwa uchi kwa lengo la kumshawishi washiriki ngono.

Humphrey Adamba alikanusha shtaka la kumtumia picha za ngono mtoto huyo kwa lengo la kumchafua mawazo.Shtaka lilisema mshtakiwa alimtumia mlalamishi picha za wanaume wakibusu wanawake mnamo Oktoba 11, 2021 kwa lengo la kuboronga mawazo yake.

Adamba mwenye umri wa miaka 20 alikanusha shtaka dhidi yake aliposhtakiwa mbele ya hakimu mkazi mahakama ya Milimani Bi Wandia Nyamu. Mshtakiwa huyo aliomba mahakama imwachilie kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda  hakupinga ombi la mshtakiwa la kuachiliwa kwa dhamana. Mahakama ilimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh200,000 na mdhamini mmoja.

Endapo atashindwa kulipa dhamana hiyo mshtakiwa alipewa dhamana ya pesa tasilimu Sh100,000. Hakimu aliagiza kesi dhidi ya mshtakiwa itajwe mnamo Novemba 1,2021 kwa maagizo zaidi.

Mshtakiwa alionyesha mshtuko alipoanza kufungwa pingu apelekwe rumande hadi pale atakapolipa dhamana.

  • Tags

You can share this post!

Bawabu taabani kwa kumpiga mwanamke picha akiwa msalani

Ni hatia kumsingizia mtu kuwa mchawi

T L