Habari Mseto

Mwanafunzi auawa baaya ya kumuua mjomba wake

November 9th, 2020 1 min read

GEORGE MUNENE NA FAUSTINE NGILA

Mwanafunzi was shule ya upili kutoka Kaunti ya Kiriyanga alivamiwa na kuuawa na wananchi Ijumaa usiku kwa madai ya kukatakata mjomba wake  na kumuua kufuatia mzozo wa kinyumbani.

Ripoti zilisema kwamba Bw Farancis Mwaniki kijana wa miaka 20 aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha nne alimvamia mjomba wake Samuel Chomba wa miaka 45 mapema usiku huo.

Shahidi aliyeshuhudia kisa hicho alisema Mwaniki amabye anaaminika kuwa alikuwa akitumia dawa za kulevya alimvamia mjombake kwa madai kwamba alikuwa mchawi.

Walitupiana maneno kabla ya mwanafunzi huyo kuchukua panga na kumkata Bw Chomba kichwani mara kadhaa huku akifariki papo kwa hapo kwenye Kijiji cha Mugambaciura.

Wakazi waliojawa na ghatahabu walivamia kijana huyo na kumrushia mawe hadi  akafariki.

Mkazi mmoja Bw Peterson Mugambi alieleza jinsi alizuia kijana huyo kuvamia mjombake bila mafanikio.

“Hatukufikiri kwamba mwanafunzi huyo angetenda kitendo kama hicho,” alisema Nancy Wathuki.