Mwanafunzi awaua wazazi wake chuoni na kutoroka

Na MASHIRIKA

MICHIGAN, AMERIKA

MWANAFUNZI mmoja wa chuo kikuu Jumamosi aliwaua kwa kuwapiga risasi wazazi wake chuoni mwake katika jimbo la Michigan kabla ya kutoroka, maafisa walisema.

Kisa hicho kilichotokea asubuhi kilisababisha taharuki chuoni humo na kupelekea wanafunzi kujifungia madarasani na kwenye mabweni wakihofia maisha yao.

Mwanfunzi huyo kwa jina Eric Davis, 19, bado anasakwa na maafisa wa polisi.

Polisi wanasema mwanafunzi huyo alimuua babake, ambaye ni afisa wa polisi, na mama yake, ndani ya bweni la chuo hicho “baada ya kugombana kuhusu masuala ya kinyumbani”.

Hakuna majeruhi wengine walioripotiwa.

Chuo hicho ambacho kiko katika mji wa Mount Pleasant, Michigan, kilifungwa mwendo wa saa mbili na nusu asubuhi.

Kisa hicho kinajiri siku chache baada ya mwanafunzi mmoja wa shule ya upili jimboni Florida kuwaua watu 17 kwa risasi.

 

Habari zinazohusiana na hii

Nani huyo kawanyonga?