Kimataifa

Mwanafunzi taabani kwa kupandikiza bangi kwa stroberi

November 12th, 2018 1 min read

MASHIRIKA NA PETER MBURU

MWANAFUNZI wa chuo kimoja Marekani amekamatwa na polisi, kwa kosa la kuzalisha mimea ya kupandikiza kutokana na mimea ya bangi na stroberi kwa maonyesho katika somo lake.

Mwanafunzi huyo wa miaka 24 katika idara ya Bayolojia, Chuo Kikuu cha Miami anasemekana kuwa mpenzi wa mmea wa bangi kwa muda mrefu, hadi kumpelekea kufanya uzalishaji huo.

Lakini alieleza polisi kuwa hajawahi kutumia bangi akisema “sijawahi kuvuta hata pafu moja, niliona tu itakuwa vyema kufanya uzalishanaji wa mimea hii miwili namna tu huwa kuna bidhaa za tumbaku zilizowekwa utamu.”

Inadaiwa kuwa mwalimu wake alishtuka alipoona hivyo na kuripoti mara moja kwa mwalimu mkuu. Kisa hicho kilikifanya chuo kuripoti kwa mamlaka ya nchi, ili kuokoa jina lake lisichafuliwe.

Japo polisi walifanikiwa kuuchukua mmea huo, haikuwa kwa njia rahisi kwani wanafunzi wengi walikuwa wakiutak.

“Baadhi ya wanafunzi wa darasa langu walichangamka, walitaka kukata matawi kadha na kuunda misokoto lakini polisi wakafika haraka. Natumai kuwa haki itatendeka na inihurumie kwani sina makosa, mimi ni mwanafunzi.”