Mwanagofu Kibugu ala Sh0.6 milioni Magical Kenya Open

Mwanagofu Kibugu ala Sh0.6 milioni Magical Kenya Open

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Mutahi Kibugu alijihakikishia tuzo ya Sh616,153 baada ya kumaliza mashindano ya kimataifa ya gofu ya Magical Kenya Open katika nafasi ya 65 uwanjani Muthaiga, Nairobi, Jumapili.

Kibugu alikamilisha kwa pointi 283 baada kuandikisha alama 68 katika raundi ya kwanza, 71 katika raundi ya pili na pia ya tatu na 73 katika raundi ya mwisho. Alikuwa Mkenya wa pekee kufika mduara wa kupokea zawadi baada ya Dismas Indiza, Njoroge Kibugu, Greg Snow, Simon Ngige, Justus Madoya, Jaydeep Singh Sandhu, Daniel Nduva, Charles Wangai, Mike Kisia, Adel Balala, John Lejirma, Dennis Maara, Daniel Kiragu na Samuel Njoroge kubanduliwa mapema.

Mashindano hayo yalivutia zaidi ya washiriki 150 kutoka Kenya, Uhispania, Japan, Afrika Kusini, Scotland, Uholanzi, Ufaransa, Austria, Amerika, Uingereza, Italia, Ujerumani, Malaysia, Northern Ireland, Uswisi, Ureno, Denmark, Uswidi, India, Ubelgiji, Norway, Iceland, Canada, Australia, Uchina, Zimbabwe, Wales, Poland, Uganda na Ireland.

Tukienda mitamboni Mhispania Jorge Campillo alikuwa mbioni kutwaa taji baada ya kuandikisha mipigo 17 ndani ya wastani akifuatiwa na Mjapani Masahiro Kawamura (-15) na Mhispania Borja Astudillo (-13). 

Bingwa wa 2022 Ashun Wu kutoka Uchina aliondolewa katika raundi ya pili. Wanagofu 65-bora wanapokea zawadi katika raundi hiyo ya 14 kati ya 39 za DP World Tour (European Tour). Wataokamilisha tatu-bora watatia mfukoni Sh43.6 milioni, Sh28.2 milioni na Sh16.0 milioni mtawalia. Kampuni ya Nation Media Group imekuwa ikisaidia shughuli za gofu nchini ikiwemo Magical Kenya Open.

  • Tags

You can share this post!

Majangili wazua hofu bila kujali wanajeshi

Ruto, Raila wazidi kuzozana huku wakiambiwa wakae wazungumze

T L