Kimataifa

Mwanamitindo aliyenyolewa rasta gerezani apatwa na matatizo ya akili

Na NA MASHIRIKA June 20th, 2024 1 min read

KAMPALA, UGANDA

MWANAMTINDO wa mavazi maarufu nchini Uganda Bw Latif Madoi, amepatwa matatizo ya akili baada nywele zake ndefu (rasta) kunyolewa katika gereza la Kasangati.

Bw Madoi, 47, alikamatwa NA polisi Mei 13 na wanafunzi wake wanne akiwa kwenye shule anayomiliki ya utaalamu wa mitindo.

Alishtikiwa kwa kumiliki sare za wanajeshi na polisi kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria za Uganda.

Kulingana na Wakili wake Bw George Musisi alisema haamini mavazi hayo yalitoka kwa shule ya mteja wake, akitaka polisi kuwasilisha ushahidi.

“Mteja wangu ana matatizo ya akili baada ya kukatwa nywele zake ndefu ambazo alitumia miaka 17 kuzikuza. Nywele hizo zilikuwa muhimu kwa utambulisho wake Bw Madoi,” alisema Bw Musisi.

Kukata nywele ni utaratibu wa kawaida kwa wafungwa wote nchini Uganda.

Kiongozi wa Upinzani Uganda Bw Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu Bobi Wine alimtembelea Bw Madoi gerezani.

Baadaye kiongozi huyo wa upinzani aliambia Bobi Wine, aliwaambia wafuasi wake kwamba mwanamtindo huyo amekuwa na maumivu makubwa zaidi kwa kupoteza nywele zake.

Wakosoaji nchini humo walidai Bw Madoi alifungiwa kwa sababu alitengeneza vazi (Ovaroli nyekundu, ambayo hutumiwa na wazima moto) ambalo linatumiwa na Bobi Wine kama sahihi yake.

“Ninavaa ovaroli aliyonitengenezea hadharani, kwa nini awe jela kwa kuitengeneza?” aliuliza Bw Bobi Wine.

Polisi walisema walivamia shule ya Madoi, na kupata nguo haramu zikiwemo za kijeshi, kofia na kaptula za kijani za jeshi.

Tangu mwaka 2005, kuvaa sare za kijeshi ni haramu nchini Uganda.

Hivi majuzi serikali ya nchi hiyo iliongeza mshipi mwekundu kwenye orodha ya nguo zilizopigwa marufuku ambao Bobi Wine na wafuasi wake huvalia.