Habari Mseto

Mwanamke afariki baada ya kulala chumba kimoja na shemeji yake

September 28th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Mwanamke wa Nairobi amefariki Alhamisi asubuhi baada ya kulala chumba kimoja hotelini na shemeji yake.

Mwanamke huyo wa miaka 42 alifariki  alipofikisha hospitalini Kenyatta alipokimbizwa baada ya kupatwa na matatizo.

Polisi walisema kwenye ripoti waliyotoa kwamba shemeji ya mwanamke huyo alikuwa amesafiri kutoka Malindi hadi Nairobi siku iliyotangulia.

Alipowasili Nairobi saa moja na nusu usiku alitafuta chumba alicholala akiwa  na shemeji yake kwenye hoteli ya Graceland barabara ya Dubois.

“Mwanamke huyo alipata matatizo  ya kukohoa na kutapika.” ilisema kauli ya polisi. Shemejiye alichukua taxi aliyompeleka kwenye Hospitali ya Kenyatta ambapo alifariki alipofika na kisa hicho kuripotiwa kwa polisi nambari ya OB 14\24\92020.

Mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali ya Kenyatta uchunguzi ukiendelea kubaini kilichosababisha kifo hicho.