Habari Mseto

Mwanamke ajuta ngozi yake kufanana na ya chui akijaribu kuibadilisha rangi

October 19th, 2018 1 min read

Na PETER MBURU

MWANAMKE mmoja amegeuka ngozi na kufanana na chui, baada ya kutumia mafuta ya kubadili ngozi rangi, lakini yakamwendea vibaya.

Bi Owethu Mlilo alisema ngozi yake ilianza kupata madoadoa baada ya kujipaka mafuta aliyopendekezewa na rafikiye, baada ya kujaribu kutumia mengine mara nyingi lakini yakakosa kumrembesha alivyotaka.

Mwanamke huyo alisema rafikiye ambaye mbeleni hakuwa na sura ya kuridhisha sana alibadilika na kuwa mrembo kupindukia, na kuwa alipompendekezea mafuta hayo alisema ni hayo yaliyomridhisha.

“Nilikuwa nimejaribu mafuta aina tofauti mbeleni na hakuna yaliyonisaidia. Rafiki yangu alinishauri kujaribu mafuta hayo mapya aliyosema yataleta matokeo ya haraka nay a kuridhisha,” akasema Bi Mlilo.

Alisema baada ya kuyatumia alianza kutpoka madoadoa meusi kwenye ngozi lakini akadhani ni adhari kidogo, kabla ya hali kuharibika na madoadoa hayo kuongezeka weusi na ukubwa.

Yalipomjaa mwilini, mwanamke huyo alihofia na kuwacha kutumia mafuta hayo kabisa, lakini yakawa tayari yamemwadhiri kwani hadi sasa yuko katika hali hiyo.

Kisa hiki kinakuja wakati idadi ya wanawake wanaotafuta urembo kwa kutumia mafuta ya kujibadili rangi ngozi zao inazidi kuongezeka

“Kwa sasa inanibidi kuvalia nguo zinazokinga kila sehemu ya mwili, kuvalia kofia n ahata miwani. Hata ninawazia kuanza kuvalia buibui,” akasema.

Anasema hali hiyo sasa imemfanya kujutia, huku akiwashauri wanawake kujivunia ngozi yao ilivyo, japo anapokea matibabu kutokana na hali ya ngozi iliyompata.