Kimataifa

Mwanamke alia kugundua mumewe ana 'jembe' ndogo

February 13th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMKE kutoka ughaibuni amejitokeza kulalamika mitandaoni kuwa mumewe waliyeoana majuzi alimhadaa, baada ya kusubiri hadi wafunge ndoa ili kufanya ngono, japo baada ya kufunga ndoa alibaini kuwa mwanamume huyo ana kiungo kidogo kupita kiasi cha uume.

Mwanamke huyo wa miaka 27 alisema alibaini hivyo walipokuwa wakisherehekea fungate (hanimuni), ambapo walipotaka kufanya mapenzi aligundua kuwa uume wa mpenzi wake ulikuwa mdogo ajabu.

Alisema alihisi kusalitiwa na akakasirika sana, hivi kwamba aliamua kutoboa siri za kitandani kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema kuwa kila alipomtaka wafanye ngono walipokuwa katika uhusiano kabla ya kuoana, mwanamume huyo kila mara alitoa vijisababu, akisema alitaka waoane kwanza ili washiriki.

“Tulikuwa na uhusiano kwa miezi sita na tukapanga kuoana kwa miezi sita mingine. Niliolewa Jumamosi iliyopita na nimetoka fungate saa chache tu zilizopita,” akasema.

Alisema kuwa japo mumewe hajaokoka, alikuwa akisisitiza kuwa ana imani za kikale kuwa mtu hafai kufanya ngono na mtu ambaye hawana uhusiano.

“Nilijaribu kumsukuma tufanye mapenzi lakini kila mara alinikanya nilipokaribia kufika hapo,” akasema.

Alisema kwamba baadaye alibaini kuwa uume wa mwanamume huyo una urefu wa kama inchi moja na robo, jambo ambalo lilimkasirisha.

“Sikuonyesha kuwa kulikuwa na chochote kibaya japo hata tulipokuwa tukitembea mjini, nilihisi kuwa kila kitu hakikuwa sawa. Nahisi nilidanganywa, ama nilifichwa kitu akifahamu tu. Sikutarajia hivi kabisa,” akasema.

Watumizi wa mitandao walichangamkia mjadala baada ya mwanamke huyo kuchapisha ujumbe huo, kila mtu akiwasilisha wazo lake.