Kimataifa

Mwanamke aliyebakwa na mumewe auawa

October 3rd, 2018 1 min read

Na AFP

TEHRAN, IRAN

TINEJA aliyebakwa na mume wake, aliuliwa Jumanne baada ya kuhukumiwa kifo, shirika la kutetea haki za kibinadamu la Amnesty International lilisema.

Zeiban Sekaanyand, kutoka jamii ya Wakurdi, alikuwa na umri wa miaka 15 wakati alipoozwa miaka tisa iliyopita. Alifungwa gerezani miaka miwili baadaye kwa kumdunga kisu mume wake na kumuua akasema alikuwa anajaribu kumbaka.

Sekaanyand, ambaye pia alifuchua kuwa shemeji yake alikuwa akimbaka mara kwa mara, alikuwa na umri wa miaka 24 alipouliwa.

Ingawa awali alikuwa amekiri kumuua mke wake, baadaye alipopata wakili alibadilisha ushuhuda huo na kusema alilazimishwa kusema hivyo na polisi.

Kulingana naye, ni shemeji yake, ambaye pia alikuwa akimbaka, aliyemuua mume wake.

 

-Imekusanywa na Valentine Obara