Habari Mseto

Mwanamke aliyeishi na mwalimu apewa idhini kumiliki mali iliyoachwa na mwendazake

October 5th, 2020 1 min read

NA JOSEPH OPEDA

Mwanamke aliyeishi na mwalimu kwa miaka 30 ameruhusiwa kuzika mwili wa mwalimu huyo baada ya korti kuthibitisha kuwa hiyo ilikuwa ndoa.

Mahakama ya Eldama Ravine ilisema kwamba Bi Alice Wangui ndiye atamiliki mali iliyoachwa na Bw Nyogote Maina.

Maamuzi hayo ya korti yalifikisha mwisho mzozo kati ya Bi Wangui na wazazi wa Bw Nyogote Bi Damaris Mwihaki Njatha na ndugu wake Joseph Muroro kuhusiana ni nani anapaswa kuzika Bw Nyogote Maina.

Jamaa za Bw Nyogote alienda kortini kusimamisha Bi Wangui kumzika mwalimu huyo.

Bw Maina alifariki akiwa nyumbani kwao Eldama Ravine. Alikuwa amesafiri kuenda kujengea mamayake nyumba hapo alipoanguka kwenye eneo la mjengo.

Alidhibitisha kufariki alipofikishwa kwenye hospitali ya Mercy Mission Agosti 25 na mwili wake kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti. site.

Lakini matayarisho ya mazishi kwanza yalisimamishwa wakati Bi Wangui akipewa amri ya korti y ana Bi Njatha ikimzuia kuuzika mwili huo.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA