Mwanamke amwagia mpango wa kando Petroli

Mwanamke amwagia mpango wa kando Petroli

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE aliyemmwagia mafuta ya petroli mtaalam wa lishe katika Gereza kuu la Kamiti na kutisha kumuua kwa kumtekeza kwa moto akidai alikuwa na uhusiano na mumewe alifikishw Ijumaa katika mahakama ya Milimani Nairobi.

Upande wa mashtaka unadai Sheila Andayi Okwomi aliapa kumfundisha adabu Nancy Wanjiru Njeri kwa madai alikuwa amemnyang’anya mume. Sheila alikanusha mnamo Aprili 8,2021 alijaribu kumuua Nancy kwa kumtupia mafuta ya Petroli ndani ya Gereza kuu la Kamiti.

Alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu Bi Wendy Kagendo Michemi. Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana akisema,atatii masharti atakayowekewa na mahakama. Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda hakupinga ombi hilo la mshtakiwa kuachiliwa kwa dhamana.

Hata hivyo, Bw Gikunda aliomba mahakama itilie maanani shtaka linalomkabili mshtakiwa adhabu yake ni kifungo cha maisha akipatikana na hatia. “Shtaka linalomkabili mshtakiwa adhabu yake ni kifungo cha maisha akipatikana na hatia. Naomba korti imwachilie kwa masharti makali,” Bw Gikunda alieleza mahakama.

Bw Gikunda aliongeza kuomba mahakama imwamuru mshtakiwa asiwavuruge mashahidi kwa njia yoyote ile atakapopewa nakala walizoandika katika idara ya uchunguzi wa uhalifu sugu katika afisi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI).

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh600,000 pesa tasilimu. Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 14,2021 kwa maagizo zaidi.

You can share this post!

Uhaba wa mboga dukani ulimpa kichocheo cha kujitosa katika...

Wazalendo: Tulipata mafunzo kwa kupigwa kwa hivyo...

T L