Habari Mseto

Mwanamke aliyedai kupapaswa makalio asubiriwa kortini

April 23rd, 2019 1 min read

Na Charles Wanyoro

MAHAKAMA ya Maua Jumanne ilikataa kuondoa kesi ambapo muuzaji miraa ameshtakiwa kwa kupapasa makalio na matiti ya mwanamke hadi pale mlalamishi atakapofika kortini na ajieleze kuwa anataka Na Charles Wanyorokutamatisha mashtaka hayo.

Hakimu Mkuu Mkaazi wa Maua Oscar Wanyanga alikataa kuidhinisha barua iliyoandikwa na mshtakiwa Nkunja Bathali iliyodai amesamehewa kosa lake akisema hilo lazima lidhihirike kwa vitendo.

“Amekubali kuondoa kesi,” Bw Bathali alieleza korti.

Inadaiwa mchuuzi huyo wa miraa alimpapasa mwanamke huyo bila idhini yake katika soko la Meeria, Kauntindogo ya Igembe Kaskazini Disemba 8, 2018.

Ingawa hivyo, Bw Wanyanga alisema mahakama haiwezi kuthibitisha madai ya mshtakiwa.

Kesi itasikizwa Mei 17 ili mwanamke huyo afike kortini na kuondoa kesi hiyo jinsi alivyodai Bw Bathali.