Mwanamke aondoa kesi dhidi ya Linturi

Mwanamke aondoa kesi dhidi ya Linturi

NA RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE ameondoa kesi ya jaribio la ubakaji dhidi ya waziri mteule wa kilimo, Mithika Linturi siku chache tu kabla ya seneta huyo wa zamani wa Meru kupigwa msasa na bunge.

Hakimu Mkuu wa mahakama ya Milimani, Susan Shitubi alifutilia mbali kesi hiyo alipofahamishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kwamba Bw Linturi na mwanamke huyo wamesikilizana na kusuluhisha kesi hiyo nje ya mahakama.

Bw Linturi alishtakiwa mwaka 2021 kwa madai ya kumdhulumu kimapenzi mwanamke huyo alipoingia ndani ya chumba alichokuwa amekodisha kulala katika hoteli moja mjini Nanyuki.

Kiongozi wa mashtaka, Nyakira Kibera alimthibitishia Bi Shitubi kwamba mlalamishi aliwasilisha taarifa kuondoa kesi hiyo.

  • Tags

You can share this post!

JIJUE DADA: ‘Kuchomeka’ wakati wa kukojoa...

Wakenya kuanza kula mahindi yaliyokuzwa kutumia mbinu ya GMO

T L